Tuesday, March 4, 2014




JE! UNAJUA SUMU YA NYUKI INAVYOANGAMIZA VVU.?

Habari njema kutoka kwa wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba washington,marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili wa nyuki iitwayo TOXIN MELITTIN inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu VVU (Virusi vya ukimwi) pasipo kuacha madhara katika chembe hai za mwili.


Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya vvu iliyotolewa mwaka 2013.


Dk Hood anaeleza kuwa Sumu hii ya nyuki ya melittin imeonyesha uwezo wa kupambana na vvu kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi kwa kulitoboa tundu ktk ganda la kirusi na kuchana ganda lote hivyo kirusi huweza kuvujwa.


Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia Dk samweli wicline profesa wa biochemia wa taasisi ya Russel Hornsby anafafanua kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa na sumu ya nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye saratani.


Dk Hood anasema tena kuwa sumu hii ya nyuki inauwezo wa kitiba wa aina 2 ktk kutibu na kuzuia:-


1). kutumika kama maji mazito ya kuweka ukeni ( vaginal jelly) ilikuzuia maambukizi ya vvu kuenea.


2). kutumika kwa maambukizi ambayo tayari yapo mwilini hapa sumu ya melittin itadungwa mwilini na kuingia ktk mzunguko wa damu inaweza kuviangamiza vvu.

No comments:

Post a Comment